BURIANI

‘Jumaa tarehe saba, mbalamwezi ni ya nane,

Ngeu ikatiririka, machozi kabubujika,

Sote tuliduwiaa, kwa kupigwa na butwaa,

Vioo vilitpaka’, kwa majonzi na simanzi,

Kuishi sio lazima, ilhali ni kwa bahati.

Shababii kwa shaibu, sote tulijiandaa,

Tayari mfano wa simba, kuikabili hujuma,

Matumbo ‘likereketa, nazo nyuso zikanuna,

Tukatema balaghamu, kulishtumu janga,

Kuishi sio lazima, ilhali ni kwa bahati.

Maadili kenda wapi, sote tukalia ng’oa,

Weshimiwa kauwawa, fukara wasisalie,

Ahera kenda wote, wasio hata hatia,

Wehu hawa namna gani, kalitenda ovu hili

Kuishi sio lazima, ilhali ni kwa bahati.

Tamatio kawaidi, ‘kiuliza sala hili,

Rabana ni kwa ninio, janga hili katukumba,

Kaungana kwa umoja, pasi kufaia dafu,

Buriani kapeana, yamkini shingo upande,

Kuishi sio lazima, ilhali ni kwa bahati.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: